WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akikabidhiwa ripoti ya pili ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Masuala ya Kisheria na Kiuchumi Kuhusiana na Mchanga wenye Madini unaosafirishwa nje ya nchi yakiwemo makontena 277 yaliyozuiliwa na Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam, baadhi ya viongozi waliotajwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine kuisababishia upotevu wa fedha Serikali wametakiwa kufikishwa katika vyombo vya dola kuhojiwa na kuchukuliwa hatua mara moja.
Ripoti hiyo chini ya Mwenyekiti Profesa, Nehemiah Eliakim Osoro imebaini madudu makubwa ya makubaliano ya kimkataba kati ya Serikali na Makampuni yanayochimba madini nchini yaliofanywa na viongozi na watendaji na kulisababishia taifa kupoteza kiasi kikubwa chafedha tangu mwaka 1998 hadi 2017. Imependekeza viongozi wote waliotajwa kufikishwa katika vyombo vya sheria na hatua kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na mikataba hiyo kupitiwa upya ili iwe na maslahi ya wazi kwa taifa.
Miongoni mwa viongozi waliotajwa katika ripoti hiyo ambayo, Rais ameunga mkono asilimia 100 kushughulikiwa ni pamoja na wanasheria wa kuu wa Serikali, Andrew Chenge, J. Mwanyika, Felix Mrema, Mkurugenzi Idara ya Mikataba, Mary Ndosi, Kamishna Dalali Peter Kafumu, Mawaziri Prof. Muhongo, Daniel Yona, Abdullah Kigoda, Karamagi, William Ngeleja, Jaji Julius Malaba na Baadhi ya Maofisa wa TRA. Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti Profesa Nehemiah Eliakim Osoro imebaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na maelezo kutoka ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA) kuwa kampuniya Acacia Mining Plc haikusajiliwa.
Makampuni yanayochimba madini nchini ambayo kamati pia ilifanya mazungumzo nayo wakati wa uchunguzi wake ni pamoja na Migodi ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Acacia Gold Mining Plc), Pangea Gold Mine Ltd (Acacia Gold Mining Plc), North Mara Gold Mine Ltd (Acacia Gold Mining Plc), Geita Gold Mine Ltd(AngloGold Ashanti Ltd); jumla ya makontena 277 yamezuiliwa bandarini kujiridhisha na taarifa zilizotolewa kabla ya kusafirishwa kwake.
Mapendekezo
Mheshimiwa Rais,
Kutokana na uchunguzi, Kamati Maalum imebaini kuwa
kuna ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu mkubwa wa
mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini
yanayosafirishwa nje ya nchi. Kamati hii inatoa
mapendekezo kwa Serikali kama ifuatavyo:
1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za
kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo
imekuwa inaendesha shughuli zake nchini kinyume na
matakwa ya Sheria.
2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni
yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kodi na
mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.
3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya
nchi mpaka hapo makampuni ya madini yanayodaiwa
yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa mujibu
wa sheria.
4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa
kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia (smelter) ili
kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira
kwa watanzania.
5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria
dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa
Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za
mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa
Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa
Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia
mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za
uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni,
watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji
wa makinikia(Freight Forwarders(T)Ltd na makampuni ya
upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina
upotoshaji.
6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba
ya asilimia 90 na kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa
baadaye wakati makampuni hayo ya madini huyauza
madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.
7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa
Watumishi wa idara ya walipakodi wakubwa katika
Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia
madai ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi
na Mahakama zimekwisha yatolea uamuzi na vilevile
ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya
Kodi kwa kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda
mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua muda mrefu
kukamilika katika vyombo hivyo.
8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za
kigeni yanayotokana na mrahaba kwa mauzo ya
madini.
9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya
migodi na viwanja ndege vilivyopo vigodini ili kudhibiti
vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa na
makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.
10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa
makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Madini na Sheria za
Kodi.
11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano
na mikataba (expert in negotiation and contract)
wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji madini
ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni
ya madini ili kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa
na tija kwa taifa na badala yake kuweka masharti
yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi
ya nchi;
12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa
ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote
ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze Serikali kufanya
majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika
makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata
mapato zaidi na ushiriki katika maamuzi muhimu katika
biashara ya madini.
13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya
usafirishajibidhaa nje ya nchi kupitia bandari kama
ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili
kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya
ukwepaji kodi.
14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya
watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi
wa Rais kwa manufaa ya watanzania.
15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya
uchimbaji mkubwa wa madini (Mining Development
Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge
kabla ya kuanza kutekelezwa.
16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe
uhuru wa mamlaka ya (discretionary powers) za Waziri
wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na maafisa
madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji
madini.
17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa
leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini lazima yaoneshe
mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo
kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama
wataalam na kuchukua nafasi za uendeshaji wa migodi
husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam
kutoka nje ya nchi.
18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha
zinazotokana na mauzo ya madini katika benki zilizopo
nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa mianya
ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.
19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na
kubadili kabisa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili
kuondoapamoja mambo mengine masharti yote
49
yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na
masharti yaliyomo kwenye kifungu thabiti (stability
provision).
20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa
Serikali ili kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya
majadiliano na uendeshaji wa mashauri yatokanayo na
mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in
negotiation and arbitration).
21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi
wa mara kwa mara kaw makampuni ya madini ili
kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa Sheria na
taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.
Mheshimiwa Rais,