Mwamuzi mmoja wa mpira wa miguu nchini Uturuki aliyefutwa kazi kwa tuhuma kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja, ameshinda kesi dhidi ya shirikisho la soka la Uturuki.
Mahakama nchini Uturuki imeamuru shirikisho hilo kumlipa refa huyo dola 8,000 kama fidia.
Halil Ibrahim Dincdag amefurahia ushindi huo mahakamani na kusema kuwa ni ushindi kwa watu wanaobaguliwa kijinsia haswa katika michezo nchini Uturuki.
Bwana Dincdag sasa amesema atarejea mahakamani kuitaka shirikisho hilo la soka kumrejeshea leseni yake ya kazi.
Shirikisho kwa upande wake limejitetea likisema kuwa Dincdag alifutwa kazi kwa sababu ya ”upungufu wa kitaaluma”
Dincdag alikuwa akiendesha mechi katika daraja la pili mwaka wa 2009.