Redd’s Miss Tanga, Kutembelea Vivutio June 17

mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga

WAREMBO wanaowania umalkia wa Mkoa wa Tanga “Redd’s Miss Tanga 2013”wanatarajiwa kutembelea katika vivutio vya utalii na maeneo ya kihistori yaliyopo mkoani hapa June 17 mwaka huu lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kupata fuksa nzuri ya kuweza kuutangaza kwa wageni na wenyeji.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa ambapo litapambwa na wasanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini na bongo fleva ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa huu ambao watajitokeza kushuhudia kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema kuwa warembo hao tayari wameanza mazoezi kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga ambapo wameweza kuwateka wadau wa tasnia hiyo ambao wamekuwa wakijitokeza kila siku kushuhudia mazoezi hayo.

   “Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Kigundula

Shindano hilo litaanza saa 2, usiku na kueleza kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo.

Kigundula alisema kuwa mpaka juzi warembo 10 wamejitokeza na kuanza mazoezi yanayosimamiwa na warembo hao ni Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mariam Bandawe.

Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).

“Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake”alisema Kigundula

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa na CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud’s Media
Group,  pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, Kidevu,the habari na assengaoscar.blogspot.com.