Na Cathbert Angelo, Wa Kajunason Blog
SHINDANO la Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika Alhamisi ya Juni 20 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao watachuana kumpata mrembo mwenye kipaji.
Akizungumza Mratibu wa Shindano hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.
“Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao,” alisema Ssebo.
Warembo warembo wanaotarajiwa kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na Dar Indian Ocean ambao kwa pamoja wanaunda Redd’s Miss Kinondoni 2013.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, dev.kisakuzi.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.