Real Madrid, Roma Kusaka Nafasi ya Robo Fainali Leo UEFA

DRI

Michuano ya klabu bingwa Ulaya itaendelea tena leo kwa michezo miwili kuchezwa ikiwa ni nafasi ya kusaka tiketi ya robo fainali.

Miamba wa soka wa Hispania Real Madrid, watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu kuwaalika AS Roma, ambapo Real Madrid wanashuka dimbani wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa kwanza.

real-madrid-vs-roma

Katika dimba la Volkswagen Arena huko Ujerumani VfL Wolfsburg watakipiga na Kaa Gent kutoka ubelgiji,VfL Wolfsburg wapo katika nafasi nzuri kutinga Robo Fainali baada ya kushinda Mechi za Ugenini kwa 3-2.

Michezo hii itachezwa saa 4:45 kwa saa za Afrika mashariki, Fainali ya michuano hii zitafanyika Mei 28 katika dimba la San Siro huko Milan Italia.