Na Woinde Shizza, Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka baadhi ya wanasiasa kuacha kulitumia tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu yao ya kujinufaisha kisiasa, ikiwa ni pamoja na baadhi kupotosha jamii kupitia mitandao ya kijamii. Hayo yamebainishwa jana na Gambo wakati alipokuwa akipokea rambirambi za wanafunzi 32 wa Lucky Vicent, zilizotolewa na chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja na uongozi wa shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea umaarufu.
Alisema kuwa swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha, hivyo
linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa ni jambo la kusikitisha sana kwani walikuwa wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.
“Pia napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha
kuwa jumla ya watu wote waliopata tatizo walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia ni binadamu,”alisema Gambo.
Alisema kuwa japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada wata wakumbuka na hawa majeruhi.
Kwa upande wake katibu mku u wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi kwenda kujichanga tena kwa ajili ya
kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani
“Tumetoa hiki kidogo lakini kwa jinsi tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha zingine kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa nchini,” alisema Mmasi
Katika michango hii shule ya shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ilichanga kiasi cha shilingi milioni tatu laki moja na nusu huku chama cha wamiliki wa uzamafuta rejareja wakiwa wamechangia shilingi milioni saba laki saba huku wote wakiaidi kwenda kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya majeruhi.