RC Ataka Malighafi za Kilimo Kuuzwa kwa Gharama Ndogo!.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha pia alipata nafasi kutembelea banda linaloonyesha uzalishaji wa nyanya, hapa butwa godluck meneja masoko na mauzo akitoa maelezo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha pia alipata nafasi kutembelea banda linaloonyesha uzalishaji wa nyanya, hapa butwa godluck meneja masoko na mauzo akitoa maelezo.

Imeelezwa kuwa teknolojia duni,rasilimali fedha,malighafi kuwa juu, uhaba wa mvua unaotokana na uharibifu wa mazingira ndio changamoto kubwa inayomkabili mkulima wa Tanzania kutofikia malengo ya kufanya kilimo biashara.
hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa arusha mrisho gambo aliyewakilishwa na mkuu wa wilaya ya arusha fabian daqarro kwenye maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana agritech expro Tanzania yamefunguliwa jijini arusha ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika jijini hapo katika viwanja vya taasisi ya utafiti wa kilimo ya seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
vilevile amesema kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa siku mbili, hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wa wataalamu mbalimbali, ukaowasidia kuendesha kilimo chenye tija.

“serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”, amesema fabian daqarro.
amewataka wadau hao wa maonyesho hayo ya kilimo kuangalia namna bei za pembejeo za kilimo, kwani inaonyesha asilimia kati ya 75-80 ni ya wakulima wadogo wadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili mkulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua pembejeo hizo ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa.

kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya utafiti ya seliani amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo, katika uzalishaji wa teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.
“sisi seliani tupo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi taongezeka pamoja na wakulima watafahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wa mazao” amesema dr. mafuru.

Mshauri wa mambo ya uchumi kutoka wizara ya kilimo na chakula Profesa

Aden Nyange akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo AGRItech.

 

Alan Edwards meneja masoko kanda ya

Afrika akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian alipotembelea banda

lao mapema leo.

 

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian

Daqarro kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni tanzu

ya kilimo PASS huku meneja usimamizi maarifa na mawasiliano wa AMDT Al-amani

Mutarubukwa akisikiliza akiwa kashika kifaa kimoja kinachohusika katika kilimo.

 

Mashine saidizi ya kubebea mizigo

ambayo imetengenezwa na kampani ya BUV Tanzania, Scott Price aliyekaa juu ya

pikipiki hiyo anamuonyesha mkuu wa wilaya (kulia) jinsi inavyofanya kazi.