Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele atashiriki katika mechi dhidi ya Arsenal baada ya kukosa mechi mbili akiuguza jeraha .
Mchezaji Dele Ali aidha huenda akaanza baada ya kutumika kama mchezaji wa ziada kutokana na jeraha dogo la kifundo cha mguu.
Wakati huohuo kipa wa Arsenal Petr Cech hatocheza kwa hadi wiki nne na jeraha la mguu alilopata baada ya kugongana na wachezaji wa Swansea wakati wa kupigwa kwa kona.
Mahala pake Cech patachukuliwa na David Ospina.Vilevile beki matata wa Arsenal Laurent Koscielny naye hatoshiriki kutokana na jeraha la paja.
Naye Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester United na Swansea.
The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.
Sanchez aliongea:Iwapo tutaingia katika uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.
Mechi nyengine zitakazochezwa katika ligi ya Uingereza siku ya leo Jumamosi ni
Chelsea v Stoke
Everton v West Ham
Man City v Aston Villa
Newcastle v Bournemouth
Southampton v Sunderland
Swansea v Norwich
Watford v Leicester