Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma Mei 02,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho
Picha na Ikulu