Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43, 44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Wizara hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi kama ifuatavyo:-
1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.
2. Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora:
i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe. Haroun Ali Suleiman.
ii. Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe. Khamis Juma Maalim.
3. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ – Mhe. Haji Omar Kheri
4. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mhe. Mohammed Aboud Mohammed
5. Wizara ya Fedha na Mipango:
Waziri wa Fedha na Mipango – Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed
6. Wizara ya Afya
i. Waziri wa Afya – Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
ii. Naibu Waziri wa Afya- Mhe. Harusi Said Suleiman
7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
i. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali –Mhe. Riziki Pembe Juma
ii. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.
8. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto:
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,Wanawake na Watoto – Mhe. Moudline Castico
9. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko – Mhe. Balozi Amina Salum Ali
10. Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji:
i. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume
ii. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mhe. Mohammed Ahmed Salum
11. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi:
i. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mhe. Hamad Rashid Mohammed
ii. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mhe. Lulu Msham Abdulla
12. Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo:
i. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Mhe. Rashid Ali Juma
ii. Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis
13. Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira:
i. Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira – Mhe. Salama Aboud Talib
ii. Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma
Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa
Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum:
i. Mhe. Said Soud Said – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum
ii. Mhe. Juma Ali Khatib – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
Uteuzi huo umeanza tarehe 9 Aprili 2016.
Waheshimiwa wote waliotajwa wanaombwa wafike Ikulu Mjini Zanzibar Jumapili tarehe 10 Aprili 2016 saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.
Imetolewa na Ikulu ya Zanzibar