Rais wa Sri Lanka Awasili nchini

Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa na Rais Jakaya Kikwete wakiangalia kikundi cha ngoma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam.

Na. Lorietha Laurence –Maelezo

RAIS wa SriLanka Mahinda Rajapaksa amewasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius K.Nyerere jijini Dares Salaam.

Rais huyo aliwasili nchini majira ya saa 3:55 akiwa amebebwa na Ndege aina ya Air bus 340 akiwa na wasaidizi wake.

Aidha Rais huyo alipata nafasi ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi hayo na kufuatiwa na wimbo wa Taifa wa Sri Lanka na Tanzania , pia alipigiwa mizinga 21 ikiwa ni heshima ya kumkaribisha nchini .

Gwaride maalum likitoa heshima leo kwa Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam.Picha zote na Magreth Kinabo – maelezo

Rais huyo alipata nafasi ya kutumbuizwa na vikundi vya Ngoma za Utamaduni vilivyokuwepo uwanjani hapo na kuelekea katika gari maalum liloandaliwa kwa ajili yake na kuelekea katika Hoteli ya Serena.

Baadaye Rais huyo atembelea Ikulu jijini Dar es Salaam mnamo saa 11:00 jioni kwa ajili ya kutia saini mikataba ya kiuchumi baina ya Tanzania na Sri lanka kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi. Pia atafanya mazungumzo rasmi na Rais Kikwete na kushiriki dhifa ya kitaifa.

Rais huyo atakuwepo nchini kwa muda wa siku tatu,ambapo Juni 28, mwaka huu atatembelea Hekalu la Kibudha lililopo Upanga,jijini Dar se Salaam lililojengwa na Sri Lanka miaka 93 iliyopita.

Aidha Rais Rajapaksa anatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue)utakaofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai Mosi, mwaka huu.

Rais huyo anatarajiwa kuondoka nchini Juni 29, mwaka huu kurejea nchini kwake