Rais wa FIFA Aipendelea Bara la Afrika Kombe la Dunia

infantino

Bara la Afrika litapewa nafasi nyengine mbili zaidi iwapo ulimwengu wa dunia litaongeza idadi ya mataifa yanayoshiriki hadi 40 kuanzia mwaka 2026 kulingana na rais wa FIFA Gianni Infantino.

Infantino alipendekeza kuongezwa kwa timu hizo kabla ya kuchaguliwa kwake na shirikisho hilo la soka duniani. Kwa sasa Afrika ina nafasi tano pekee katika michuano hiyo .

Hatahivyo hatua hiyo itaidhinishwa hadi mwaka 2026 huku timu 32 zikiwa tayari zimethibitishwa kushiriki katika kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.