Rais wa Chama Cha Soka Barani Asia Atembelea Ofisi Za TFF

sheikhmalinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Asia (AFC), na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa jana ametembelea wizara ya Habari, Utamaduni, Sana na Michezo, ambapo alifanya mazungmzo mafupi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.

Katika mazugmzo hayo, Sheikh Salman ameielezea Serikali ya Tanzania nia ya FIFA kuendelea kushirikiana na Serikali na TFF katika kuendeleza programu mbalibali za maendeleo ya mpira hasa wa vijana na wanawake.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Elisante ameihakikishia FIFA kuwa nia ya Serikali ni kuona mpira unakua nchini na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TFF na FIFA ili kufikia azama hiyo.

IMG-20160118-WA0005

Aidha pia ametoa wito kwa AFC kusaidiana na TFF katika masuala ya exchange programmes ili vijana wetu wapate uzoefu wa nje.
Sheikh Salman na ujumbe wake walitembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wakiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na shirikisho, ikiwemo uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.

Kiongozi huyo wa AFC, aliwasali nchini jana mchana kwa matembezi ya siku mbili chini ya mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi na anatarajiwa kuondoka nchini leo.