Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. John Pombe Magufuli akibadilishana makabrasha ya mkataba na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji Saini wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. John Pombe Magufuli akitia saini kwenye mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akitia saini kwenye Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki.
Rais Dk. Magufuli akitoa hotuba yake mara baada ya zoezi la utiaji Saini kukamilika.