Rais Obama Awatolea Uvivu Viongozi wa Afrika…!

Rais wa Marekani, Barack Obama-marekani akizungumza.

Rais wa Marekani, Barack Obama-marekani akizungumza.


RAIS wa Marekani Barrack Obama, amewapasha viongozi wa Afrika ambao wanaendelea kung’ang’ania madarakani hata baada ya Katiba kutowaruhusu kuendelea kuwania tena nyadhifa zao za urais.

Katika hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani kwa muungano wa Afrika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, amesema kuwa Afrika haitapiga hatua iwapo viongozi wake watakataa kuondoka madarakani baada ya muda wao kuisha.

Alimtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano na anafahamika pakubwa kote duniani huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kukwamia madaraka.

Aliongeza kuwa wakati waandishi wanapofungwa huku wanaharakati wakitishwa, demokrasia huwepo tu kwa jina. Akimnukuu shujaa Nelson Mandela akisema kuwa unapoheshimu uhuru wa wengine watu wote huwa huru. Amesema kuwa ishara kuu ya maendeleo katika taifa ni vile linavyowachukulia wanawake wake.

Alibainisha kuwa viongozi wa Afrika kwamba maendeleo ya bara hili yanategemea demokrasia, uhuru na haki za kibinaadamu. Anaongeza kuwa muda umewadia wa kubadilisha mtizamo wa Afrika kama bara duni lenye kulemewa na umaskini na mizozo.

Aidha ameupongeza umoja wa Afrika AU na shirika la Umoja wa mataifa katika mapambano dhidi ya makundi ya wapiganaji wa kiislamu kama vile, Boko Haram kaskazini mwa Nigeria na Al – Shaabab Afrika mashariki.

Amemtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano huku akiacha umaarufu na kufahamika sehemu kubwa duniani na kiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kung’ang’ania madaraka.
-BBC