Rais Obama aahidi kuisadia Burma zaidi

Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za kuleta mabadiliko nchini Burma.

Katika ziara yake fupi ya kihistoria, Obama alikutana na Rais Thein Sein na kusema uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Burma kutategemea jinsi taifa hilo litakavyoshughulikia malalamishi yaliyokuwa yametolewa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.

Aidha Obama alikutana na mwanaharakati wa haki za kibinadamu na kiongozi wa upinzani, Aung San Suu Kyi.

Lakini alilaani mapigano ya hivi majuzi kati ya Wasilimu na Wabudhist huko Burma magahribi, na akatoa wito wa kujumuishwa kwa Warohingya, ambao ni Waisilamu, na ambao hawatambuliwi kama raia.

BBC