IKIWA ni siku chache baada ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, kunusurika kupinduliwa madarakani amewafukuza kazi mawaziri watatu katika Serikali yake.
Hata hivyo bado maandamano ya wananchi yanaendelea katika Mji Mkuu wa Burundi Bujumbura ikiwa ni ishara ya kumshinikiza asigombee muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Mawaziri walioachishwa kazi ni pamoja na Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Mashauri ya nchi za Kigeni na Waziri wa Biashara.
Mapema jana polisi nchini humo walifyatua risasi hewani katika Mji Mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia eneo hilo.
-BBC