Rais Mstaafu Mwinyi Awaasa Watanzania

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na watoto wanaotoka katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima vya jijini Dar es salaam, wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali wakati wa Futari aliyooiandaa jana usiku katika viwanja vya Karimjee.

Baadhi ya wananchi wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Baadhi ya wananchi wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Baadhi watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.

Baadhi watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.

Rais mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam akijumuika pamoja  na watoto hao na wageni mbalimbali walioalikwa katika Futari hiyo.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.

Na Aron Msigwa – MAELEZO

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amewataka Watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao. Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.

“Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu,” alisisitiza.

Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa  mvua jijini Dar es salaam.

Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.

Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.

Katika hatua nyingine, Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi. Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumilia.