Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi(kulia) akiangalia mahindi yaliyopandwa kitaalamu jana (leo) jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo mstaafu kutembelea bustani ya mfano ya MAGEREZA katika maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi(katikati) akiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda kutembelea mabanda mbalimbali jijini Dar es salaam katika maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi akitopata maelezo juu ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo mstaafu alipotembelea maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.