Rais Magufuli: Tanzania ni Tajiri Tatizo Mafisadi Wanaturudisha Nyuma

4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi ya Tanzania ni tajiri na inarasilimali nyingi ,ila baadhi ya matajiri ambao ni mafisadi ndio wanasababisha nchi yetu kuonekana masikini hivyo amehaidi kula nao sahani moja.

Aliyasema hayo leo wakati akiongea na wananchi wa mkoa wa Arusha waliojitokeza barabarani kumpokea huku wakimuomba aendelee kutumbua majipu.

Alisema kuwa nchi ya Tanzania ina rasilimali nyingi ila kuna baadhi ya matajiri ambao wanapenda kujilimbikizia fedha wamekuwa wakifanya ufisadi na kusababisha baadhi ya wananchi kuendelea kuwa maskini pamoja na nchi yetu kuonekana masikini .

“Nasema hivi kuanzia sasa nipo tayari kulala mbele na mafisadi wote na pia nawapa onyo kali wale walimu ambao bado wanatoza ada shuleni iwapo nitagundua mwalimu yeyote anaetoza Hela nahaidi ivi nitakula naye sahani moja ,na katika hili sitalifanyia masihara hata kidogo”alisema Rasi Magufuli

3

Aidha aliwaambia wananchi kuwa kuanzia sasa elimu ni bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari na serekali imeshaweka mipango hiyo tayari na imeanza kutumika.

Rais Magufuli aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi na kusema kuwa wakati wa kampeni umeisha , mambo ya siasa yameisha sasa ivi ni wakati wa kufanya kazi tu na sio kitu kingine.

“Nasema hivi sasa, huu ni wakati wa kufanya kazi kama nitaendelea kutumbua majipu kila mahali na sitamwonea huruma mtu yeyote mimi kazi yangu kubwa ni kufanya kazi tu na wananchi napenda kuwambia fanyeni kazi kwani hapa ni kazi tu”alisema Magufuli.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.

Rais magufuli alipokelewa na mamia ya wananchi mbalimbali ambao walijitokeza barabarani ambapo pindi tu alipotoka katika kiwanja cha wa ndege wa KIA, wananchi walikuwa wemejitokeza wengi mpaka ikamlazimu kusimama ili wananchi waongee naye,sehemu ambazo aliweza kusimama ni pamoja na kikatiti ,usa river pamoja na Tengeru.