Rais Magufuli Atoa ya Moyoni, Ni Katika Mazungumzo na Waandishi

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mahojiano tangu aingie madarakani. Mkutano huo umefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo pia umeenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akisisitiza jambo katika mazungumzo na waandishi wa habari na wahariri kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mahojiano tangu aingie madarakani. Mkutano huo umefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo pia umeenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mahojiano tangu aingie madarakani.

Msanii Mrisho Mpoto akiimbwa wimbo maalum wa kumpongeza rais kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Msanii Mrisho Mpoto akipeana mkono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiimbwa wimbo maalum wa kumpongeza rais kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo ametoa ya moyoni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aingie madarakani. Mazungumzo hayo ambayo yanaenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amesema kwa changamoto zilizopo nafasi ya uraisi anajutia kuwapo katika nafasi hiyo. Alisema alivyokuwa anaomba nafasi hiyo ni kama alikuwa anabipu na bahati simu ikang’ang’ania na kujipiga moja kwa moja.

Alisema kuna wakati anajifikiria na kushangaa ni kwanini baadhi wanagombani kwenda ikulu kwani ni sehemu ya changamoto nyingi pasipo mfano. Akijitasmini uongozi wake kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja anasema amejitahidi kubana matumizi ya Serikali yake kwa yeye kuwa mfano wa vitendo ili fedha nyingi zielekezwe katika huduma za kijamii. Alisema tangu aingie madarakani amepokea mialiko 47 yote ametuma wawakilishi na pengine kuwakilishwa na mabalozi jambo ambalo limeokoa kiasi kikubwa cha fedha.

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mahojiano tangu aingie madarakani. Mkutano huo umefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo pia umeenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mahojiano tangu aingie madarakani. Mkutano huo umefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo pia umeenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Baadhi ya viongozi walioambatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakiwa Meza Kuu katika mkutano huo.

Akifafanua zaidi alisema kati ya mialiko 47 ni mitatu tu ndio amekwenda yeye mwenyewe lakini wahusika wamekuwa wakimuelewa ndio maana Tanzania imeendelea kupokea viongozi mbalimbali wa juu wakiwemo marais kuja kufanya ziara nchini. Akizungumzia elimu alisema licha ya changamoto zinazoibuka katika mfumo wa elimu bure yapo mafanikio mazuri. Alisema serikali kwa sasa inatoa kiasi cha shilingi bilioni 18.7 kila mwezi kuendesha mfumo wa elimu jambo ambalo limewezekana kutokana na kubana matumizi na makusanyo mazuri ya fedha.

Alisema changamoto iliyopo ni ongezeko kubwa la wanafunzi tangu kuanza utekelezaji wa elimu bure kwa maeneo yote yaani Shule za msingi na Sekondari. Kwa darasa la kwanza kumekuwa na ongezeko la asilimia 84 ya wanafunzi huku kwa sekondari asilimia ya ongezeko la wanafunzi limefikia 87, lakini Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto hizo. Kwa upande wa elimu ya juu serikali imeongeza fungu la mikopo kutoka shilingi bilioni 340 hadi kufikia shilingi bilinoni 473 fedha zinazotengwa ili kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Greyson Msigwa akitoa utambulisho kabla ya Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuanza mazungumzo na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani.

Alisema lengo la Serikali yake ni kuendeleza kiuchumi Tanzania ili siku moja ianze kutoa misaada kama nchi nyingine tajiri duniani. Alisema Tanzania ina rasilimali za kujitosheleza na kinachotakiwa ni mipango mizuri ya kuzitumia na kuzisimamia ili zitumike kuiinua nchi na raia wake kiuchumi. Alisema Tanzania ina madini karibia ya aina zote na mengine ya thamani kubwa ukiachilia rasilimali nyingine hivyo kuna kila sababu ya kukua kiuchumi.

Aidha alisema hatua ya kubana matumizi ya Serikali ili fedha zitumike katika shughuli nyingine za maendeleo pia imewezesha Serikali kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na tayari imelipia nyingine tatu zinatengenezwa mbili aina ya Jet na nyingine Bombardier Q400 ambazo zitaboresha zaidi huduma za usafiri wa anga hasa sekta ya utalii ambao unaweza kuliingizia taifa fenya nyingi. Alisema hapo baadaye Serikali imepanga kununua ndege kubwa aina ya Boeing itakayo fanya safari za kimataifa ili kurahisisha usafiri wa watalii kutoka mataifa mbalimbali.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiuliza maswali kwa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi na wahariri wakiwa katika mkutano huo na Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.