Na Frank Shija, MAELEZO
BODI ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kupewa notisi ya siku thelethini (30) wawe wameanza kulipa madeni yao kabala hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na wadai sugu leo Jijini Dar es Salaam.
Badru amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo ya eleimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.
Alisema kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walinbainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.
Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanaza kulipa mikopo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.
Hatua hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia kuchukua hatua nyingi za ziada.
Hatua hizo ni pamoja na kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu waziwasilishe,kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.