Rais Magufuli Akabidhiwa Madawati na Jeshi la Magereza na JKT

2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwenye moja ya Dawati katika hafla hiyo fupi ya ugawaji wa Madawati hayo.

1

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimuonesha Rais Dk. John Pombe Magufuli sehemu ya Madawati yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikagua Madawati hayo yaliyotengenezwa na Jeshi la Magereza pamoja na Suma JKT

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.

4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakwanza kulia Mariam Elias (darasa la tatu na wapili kutoka kushoto George Samwel mwanafunzi wa darasa la tano wakiwa wanapiga makofi kabla ya tukio la ugawaji wa madawati hayo yaliyotokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge.

5

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel akimtajia Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.

6

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel akimtajia Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.

7

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Julay 13,2016

8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza mara baada ya kukabidhi Madawati.
PICHA NA IKULU