Rais Kikwete na Mzee Kawawa Watunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari Chuo Kikuu Dodoma


Chuo Kikuu Cha Dodoma Jana kiliwatunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor Honoris Causa) Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa kutambua michango yao mbalimbali katika Nyanja za siasa na sekta za elimu nchini ikiwemo kuasisi ujenzi wa Chuo hicho. Pichani Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa akimtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari Rais Dr.Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma jana.Katikati ni Makamu mkuu wa Chuo Profesa Idriss Kikula