RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA, AHANI MSIBA WA TRAFIKI ALIYEGONGWA NA GARI AZINDUA MAABARA YA UHANDISI JENI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha historia ya Uuguzi na Ukunga nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania katika bustani ya Mnazi Mmoja leo Machi 19, 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku medali mmoja ya wauguzi wakongwe nchini aliyewahi pia kuwa Mbunge na Msajili wa Wauguzi na Wakunga Mama Jitto Ram wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga katika bustani ya Mnazi Mmoja leo Machi 19, 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani msiba wa Askari wa Usalama Barabarani aliyegongwa na gari baada ya msafara wa Rais kupita jana WP 2942 Koplo Elikiza nyumbani kwa marehemu sehemu za Ununio ,leo Machi 19, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji mume wa marehemu na watoto pamoja na IGP Saidi Mwema alipokwenda kuhani msiba wa Askari wa Usalama Barabarani aliyegongwa na gari baada ya msafara wa Rais kupita jana WP Koplo Elikiza nyumbani kwa marehemu sehemu za Ununio ,leo Machi 19, 2013