Rais Kikwete kunzungumza na Wananchi leo

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kesho, Novemba 18, 2011, anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu leo kwa vyombo vya habari katika mkutano huo Rais atautumia pia kuzungumza na taifa zima kutoka Ukumbi wa PTA, Viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Taarifa zinasema hotuba ya Mheshimiwa Rais itaanza saa 10 kamili za mchana leo na itatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya utangazaji nchini. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais atazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa.