
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuzungumza na wabunge wa CCM katika kikao chake na wabunge hao kilichofanyika jana jioni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Wengine kutoka kushoto ni Spika wa Bunge, Anne Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.