Mhe. Rais Dr. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Bi. Gaudencia kabaka. (Na Mpigapicha Wetu)
Mhe. Rais Dr. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mjini Moshi Kilimanjaro jana. Wengine ni Waziri wa Kazi na Ajira, Bi. Gaudensia Kabaka (kushoto kwa Rais), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Bw. Leonidas Gama.
Mhe. Rais Dr. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimsikiliza kwa makini Mhandisi Mohamed Kimbe, wakati akitioa maelezo ya ujenzi wa Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya Rais Kikwete, kuzindua jengo hilo Moshi, mkoani Kilimanjaro jana.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisikiliza kwa makini maelezo ya Mhandisi Mohamed Kimbe kuhusu mradi wa Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya Rais kuzindua jengo hilo Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk. Ramadhan Dau.
Mhe. Rais Dr. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishikana mikono Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alipowasili mjini Moshi, jana kwa ajili ya kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la shirika hilo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Yakob Kidula.
Mhe. Rais Dr. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishikana mikono Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alipowasili mjini Moshi, jana kwa ajili ya kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la shirika hilo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Yakob Kidula.
*KILIMANJARO COMERCIAL COMPLEX
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete azindua rasmi jengo la kitega uchumi mjini moshi Mradi huu ni wa ubia kati ya NSSF, Tanzania Red Cross (TRCS), UMATI na Tanzania Girl Guides Association (TGGA).
Jengo hili lina jumla ya mita za mraba 30,050 za kupangisha. Yapo maeneo kwa ajili ya mabenki, sehemu za maduka, hoteli, kumbi za mikutano na maeneo ya maofisi. Hivi vyote kwa pamoja vitasaidia kutatua tatizo la maeneo ya biashara katika Manispaa ya Moshi
Alipokuwa akitoa historia ya mradi huu, Mkurugenzi mkuu wa NSSF Dr Ramadhan K. Dau alisema historia imeanzia tangu mwaka 2008 ambapo taasisi tatu zilizokuwa na viwanja vitatu vilivyoungana katika barabara za Agakhan na Arusha zilamua kuviendeleza viwanja hivyo kwa kuingia ubia na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii.
NSSF ilikubali kutoa fedha za kutekeleza mradi huu kwa asilimia 100 na mchango wa taasisi hizo ni ardhi. Kwa sasa jengo hili linamilikiwa na taasisi nne, ambapo NSSF inamiliki asilimia 75 na taasisi nyingine kwa pamoja zinamiliki asilimia 25. Kila taasisi imegawiwa eneo lake kwa ajili ya kulimiliki na kulitumia kwa jinsi itakavyoamua.
Alisema ujenzi wa mradi huu ulianza Desemba 2011 na umechukua miaka miwili kukamilika. Gharama za ujenzi ni shs bilioni 63.4 Hadi kukamilika.