Rais Kikwete azindua Karakana ya Precision Air Dar

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege la Precision Air, Michael Shirima akimkabidhi zawadi Rais Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi karakana ya ndege za shirika hilo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere leo jijini Dar es salaam, Karakana hiyo itakuwa ikihudumia ndege za mashirika mengine pia na kupokea wanafunzi walio kwenye mafunzo ya Uinjinia wa ndege kutoka katika vyuo vya ndani.

 

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe pamoja na wakuu mbalimbali wa shirika la ndege la Precision Air na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada ya uzinduzi.

 

Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air, Alfonce Kioko alipokuwa akitoa maelezo  wakati wakati Rais alipokuwa akikagua  Hanga hiyo, kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.


Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la ndege la Precision Air, Michael Shirima katikati mara baada ya kuzindua Karakana ya ndege za shirika hilo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air, Alfonce Kioko.

 

Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace ya Arusha, Vicent Laswai naye amehudhuria katika uzinduzi huo kama mdau wa Utalii.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Wafayakazi wa Precision Air wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.

 

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Hili ndilo jengo la Karakana yenyewe kama linavoonekana katika picha.