Rais Kikwete Ateuwa Makamishna Magereza

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza na maafisa wengine.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peter Ilomo amesema Rais amemteua Bwana John Casmir Minja kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:
Dk. Juma Ally Malewa ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na Uendelezaji wa Magereza. Bwana Deonice Lwamahe Chamulesile ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji. Gaston Sanga ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.

Fidelis M. Mboya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza na;

James B. Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Oktoba 1, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tangu tarehe 25 Septemba, 2012.