Rais Kikwete Ateuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji Mpya

Rais Kikwete Ateuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji Mpya


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
Taarifa iliyotolewa 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
Taarifa iliyotolewa 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huu, Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).