RAIS Jakaya Kikwete jana (Jumatano) alitembelea kituo cha Bagamoyo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) na kuonyeshwa kazi mbalimbali za utafiti zinazofanyika kituoni hapo. Raisi Kikwete aliisifia taasisi hiyo kwa kufanya kazi kubwa hasa katika upande wa ugonjwa wa Malaria na kujipatia sifa kubwa duniani.
Rais Kikwete akimsikiliza mtafiti wa IHI Dk. Nico Govella akimpa maelezo juu ya utafiti wake ambapo magunia ya katani yakichanganywa na kemikali fulani yanaweza kutumika kukinga wanadamu dhidi ya mbu wanaoeneza malaria.
Rais Kikwete akimsikiliza Grace Mwangoka wa IHI akimweleza shughuli mbalimbali za maabara kwenye taasisi hiyo.
Rais Kikwete akimsikiliza Joseph Madata ambaye ni mkutubi akimwelezea matumizi ya maktaba mtandao (digital library) ya taasisi hiyo.
Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa IHI pamoja na wenzao kutoka Equatorial Guinea ambao wapo kwenye kituo hicho cha Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo.