Rais Kikwete Amuapisha Msajili Mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nyenzo za kazi Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kumwapisha.

Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akisaini mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Jaji Francis Mutungi na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu, John Tendwa baada ya kumuapisha Jaji Mutungi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Agosti 26, 2013, amemwapisha Jaji Francis Sales Katabazi Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa mpya.

Jaji Mutungi anachukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu kutoka Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Sherehe za kumwapisha Jaji Mutungi zilizofanyika Ikulu, Dar es Salaam zimehudhuriwa pia na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi Fakhi Abdallah Rheno Jundu pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.