Rais Kikwete alivyoshiriki mazishi ya Albertina Sisulu

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Zambia Dk. Kenneth Kaunda na Mama Graca Machel wakiwa katika ibada ya Mazishi ya mpigani Uhuru wa Afrika ya Kusini Marehemu Albertina Sisulu iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Orlando, Soweto Juni 11, 2011. Marehemu Albertina Sisulu alikuwa mke wa mpigania uhuru wa Afrika ya Kusini marehemu Walter Sisulu. (Picha kwa hisani ya Ikulu)

Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Dk. Kenneth Kaunda wakiwa katika Mazishi ya mpigania uhuru wa Afrikaya Kusini Marehemu Albertina Sisulu yaliyofanyika katika makaburi ya Newclare, katika kitongoji cha Soweto Juni 11, 20011.