Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, wakiweka saini katika ramani ya duania inayoonyesha sehemu mbali mbali duniani ambapo Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani(American Peace Corps volunteer) linatoa huduma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu shirika hili lilipoanzishwa. Wengine katika picha aliyesimama kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo duniani, Bwana Aaron Wiliams, na kulia aliyesimama ni Mkurugenzi wa shikika hilo nchini Bi. Andrea Wojnar Diagne. Shirika la Peace Corps lilianzishwa mnamo Tarehe moja Machi mwaka 1961 na aliyekuwa Rais wa Marekani hayati John F. Kennedy. Hapa nchini jumla ya wanachama 2100 wa shirika hilo walitoa huduma mbalimbali kuanzia mwaka 1961 katika sekta za Elimu, Utunzaji waMazingira na afya. Kwasasa jumla ya wanachama 140 wa shirika hilo wanafanya kazi za kujitolea katika sehemu mbalimbali nchini wakifundisha masomo ya Sayansi, Hesabu na lugha ya kiingereza. (Picha na Freddy Maro)