Rais Kikwete afungua rasmi chuo kikuu cha UDOM leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Profesa Idrissa Kikula akimweleza jambo Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo hicho mjini Dodoma leo. Kulia ni Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo kikuu cha Dodoma.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa wakikata utepe kuashiria kuazindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ndiye Mkuu wa chuo cha Dodoma, na Dk. Bilal ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chuo hicho. .