Rais Kikwete afungua barabara ya Usagara Geita

Rais Dr. JakayaMrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Usagara Geita leo asubuhi.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 90 imejengwa kwa thamani ya zaidi Tshs.78bn/ zilizotolewa na serikali ya Tanzania.Wengine katika picha, Kutoka Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro,Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Herbert Mrango,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, Mbunge wa Misungwi ambaye pia ni naibu Waziri Sayansi na Teknolojia Charles Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu TANROADS injinia Patrick Mfugale.Picha na Freddy Maro