Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika
hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini
Marekani,Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi
Dume.
Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema
na asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo
yote ni salama. Tutaendelea kuwashirikisha taarifa ya maendeleo yake
mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani
kulijenga Taifa