Rais Kikwete Aagana na Mabalozi Wapya

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi saba walioteuliwa hivi karibuni na kuagana nao kabla hawajaripoti kwenye vituo vyao katika nchi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam. Mabalozi hao toka kushoto ni Modest Melo anayekwenda Umoja wa Mataifa, The Hague, Geneva, Mabrouk Mabrouk (Abu Dhabi – Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE), Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (Beijing, China), Anthony Cheche (Kinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), Chabaka Kilumanga (Visiwa vya Comoro), Wilson Masilingi (The Hague, Uholanzi) na Liberata Mulamula (Washington DC, Marekani). PICHA NA IKULU