Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA IKULU)
Wazee wa mkoa wa Dar es salaam wakimsikiliza Rais Mwai Kibaki wakati alipokua akizungumza nao jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa- MAELEZO
Rais wa Kenya Mwai Kibaki akizungumza na watanzania kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mwai Kibaki akiwasalimia wazee wa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kuwasili katia ukumbi wa mikutano wa PTA viwanja vya maonyesho ya sabasaba jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (katikati), makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (kushoto), waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) na viongozi wengine wa serikali wakimpungia mikono Rais wa Kenya Mwai Kibaki ishara ya kumuaga wakati akiondoka nchini Tanzania kurejea Kenya kufuatia kukamilika kwa ziara yake ya siku mbili. Picha na Aron Msigwa- MAELEZO