RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amelihutubia Taifa Usiku huu huku akitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Kesho na bendera kupepea nusu mlingoti, nchi nzima. Rais Kenyatta amesema wakenya na raia wote waliopoteza maisha katika shambulizi la ugaidi watakumbukwa siku zote na majeruhi wanaombewa wapone haraka na kurudi katika hali yao ya kawaida.
Miongoni mwa dondoo katika hotuba ya Rais Kenyatta ni kama ifuatavyo:- Taarifa kamili ya idadi ya watu waliouwawa katika uvamizi huo wa kigaidi Jengo la Westgate ni 62 huku 175 kujeruhiwa. Wanajeshi 3 kutoka Jeshi la KDF wameuwawa pia wakipambana na magaidi hao.
Magaidi watano wameuwawa pia katika shambulizi hilo huku watu 11 wakikamatwa kuhusika na shambulizi hilo. Pongezi kubwa zimetolewa kwa Marais wote walioitakia pole Kenya katika kipindi hiki, Wakenya kwa umoja waliouonesha kipindi chote, Viongozi wote kwa umoja waliouonesha na mataifa anuai ya jirani na mengine.