RAIS Wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa wakuu Wa Mikoa na Wilaya. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari walioteuliwa nafasi za ukuu wa mikoa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud, Mkuu Wa Mkoa Wa Kaskazini Unguja, Vuai Mwinyi Mohamed. Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa wakuu Wa mikoa ambao mikoa yao haikutajwa watakuwa wanaendelea na nyadhifa zao.
Kwa upande wa wakuu Wa Wilaya walioteuliwa ni pamoja na Mkuu Wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas, Mkuu Wa Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mhe. Silima Haji Haji, Kaskazini ‘A’, Hassan Ali Kombo, Kaskazini ‘B’, Issa Juma Ali, Wilaya ya Kati, Mashavu Sukwa Said, Mkuu Wa Wilaya ya Kusini, Idrissa Kitwana Mustafa, Mkuu Wa Wilaya ya Chakechake, Salama Mbarouk Khatib. Hata hivyo wakuu Wa Wilaya ambao Wilaya zao hazikutajwa pia wanaendelea na nyadhifa zao kama ilivyokuwa.