Leo Dk. Magufuli amemteuwa Dk Tulia Ackson Mwansasu kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dk. Mwansasu ambaye awali alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo pia alikuwa ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, anakuwa ni mbunge wa kwanza kuteuliwa na Rais Magufuli.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 66(1)(e) inampa mamlaka Rais kuteuwa wabunge wasiozidi 10 ambao anaona wanafaa na wanaweza kumsaidia kazi. Tayari Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah amekiri katika taarifa yake kwa umma kupokea jina la Dk. Tulia Ackson Mwansasu toka kwa rais na anatarajiwa kuapishwa mara bunge litakapoanza shughuli zake kesho.