Rais Dk Magufuli Amwaga Neema kwa Waliokuwa Wakazi Nyumba za Magomeni Kota

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wazee waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota mara baada ya kuzungumza nao jijini Dar es salaam. Rais pamoja na mambo mengine ameahidi kuzishughulikia kero zote za wazee hao ikiwemo kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ambazo watakaa bure bila kulipia kwa muda wa miaka 5 na baadaye kufanyika utaratibu wa kuwamilikisha nyumba hizo kwa gharama nafuu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wazee waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota mara baada ya kuzungumza nao jijini Dar es salaam. Rais pamoja na mambo mengine ameahidi kuzishughulikia kero zote za wazee hao ikiwemo kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ambazo watakaa bure bila kulipia kwa muda wa miaka 5 na baadaye kufanyika utaratibu wa kuwamilikisha nyumba hizo kwa gharama nafuu.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika nyumba za Magomeni Kota ambazo zilivunjwa kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi na Biashara ambao walitelekekezwa kwa muda mrefu na manispaa ya Kinondoni na kuwafanya waishi maisha magumu. Katika hotuba yake Rais ameahidi kuwajengea nyumba  za kisasa wakazi hao  644 ambapo wataishi  bure kwenye nyumba hizo  kwa muda wa miaka 5 kabla ya kuandaliwa kwa utaratibu wa kuwamilikisha nyumba hizo. 
 Baadhi ya wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli mara baada ya kuahidi kuzipatia majibu kero zao za muda mrefu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza jambo na viongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kuwasili eneo la Magomeni Kota zitakapojengwa nyumba za kisasa za wakazi 644   watakaojengewa nyumba hizo na Serikali. Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimweleza jambo  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (katikati) wakati akikagua eneo zitakapojengwa nyumba za kisasa za wakazi 644 wa eneo la Magomeni Kota ambao watajengewa nyumba na Serikali. Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu. Wengine Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi, Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda wa pili kutoka kulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli.

Baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es salaam wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Magomeni Kota.

 

Msemaji wa Wazee wa Magomeni Kota Mchungaji John Raymond (wa pili kutoka kushoto) akiwa na uso wa furaha akiwa  na Wakazi wenzake 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota ambao wameahidiwa kujengewa nyumba zao na Serikali.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota ambao ambao nyumba zao zilivunjwa kupisha ujenzi wa mradi wa kisasa wa Makazi na Biashara chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni. Serikali  imeahidiwa kuwajengea  nyumba wakazi hao kufuatia agizo la Rais.
 Baadhi ya akina Baba waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kufuatia kero na Hoja zao za muda mrefu kupatiwa majibu.
  Baadhi ya Wazee waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakimwombea dua ya Afya njema na Utumishi mwema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kufuatia  Hotuba kufuatia hotuba aliyoitoa mara baada ya kuwatembelea eneo la Magomeni Kota kuji kero na Hoja zao za muda mrefu huku akiahidi kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ambazo watakaa bure kwa muda wa miaka 5 kabla ya kufanyika utaratibu wa kuwamilikisha kwa gharama nafuu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alipowatembelea wakazi hao kwa lengo la kuzungumza na kujibu kero zao za muda mrefu leo jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi akizungumza na Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi akizungumza na Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota. Picha/Aron Msigwa.