Raia Wafurika Mali Kuona Muujiza Nje ya Ukuta wa Choo

Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni kuangalia picha ya muujiza huo.

Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni kuangalia picha ya muujiza huo.

Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni kuangalia picha ya muujiza huo, huku askari wakiangalia usalama kutokana na idadi kubwa ya raia.

Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni kuangalia picha ya muujiza huo, huku askari wakiangalia usalama kutokana na idadi kubwa ya raia.

Baadhi ya raia wakionesha ukuta ulio na picha hiyo.

Baadhi ya raia wakionesha ukuta ulio na picha hiyo.


UMATI wa raia umeendelea kufurika eneo moja la Mji Mkuu wa Mali, Bamako ili kujionea kile kilichotajwa kuwa ni muujiza wa kidini kwenye ukuta mmoja ambao umeonekana wiki iliopita. Idadi kuwa ya watu wanaamini picha hiyo nyeupe nje ya ukuta wa choo inamuonesha mtu akisali na kuonekana kama ishara ya ujumbe wa Mungu.

Maofisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia walipelekwa katika eneo hilo ili kudhibiti umati huo kwa kuwa watu wanapiga foleni usiku kucha kuona muujiza huo wa alama. “Tunaamini ni maono ya mtume wetu,” alisema Aliou Traore ambaye ni mkazi wa eneo hilo.

“Watu wamekuja kutoka Senegal kujionea huku baadhi ya mawaziri wa Mali pamoja na viongozi wa dini wakitutembelea kuona muujiza huu,” alisema. Bwana Traore alisema kuwa alama hiyo imekuwa ikibadilika tangu ionekane mara ya kwanza. “Mara nyengine alama hiyo inajifuta na kuonekana katika maeneo mengine ya nyumba hizi. Baadaye inarudi,” alisema.

Taarifa kutoka eneo hilo zinasema watu hawalipi chochote kuona alama hiyo lakini wanaacha fedha katika ndoo, ambazo familia ya Traore inasema itazitoa kwa msikiti wa eneo hilo. Alama hiyo inaonekana mithili ya kovu la saruji la mwanamke aliyesimama. Picha za alama hiyo zimesambaa mjini Bamako kwa kupitia simu za mkononi tangu ionekane siku ya Jumamosi.

“Ni muujiza, nimeuona,” alisema mwalimu wa shule ya msingi, Aboubakar Diarra baada ya kuona ukuta huo. “Ni kweli. Ni alama kutoka kwa Mungu kwa Mali, taifa letu ni kubwa.” Wafuasi wa Tijani ambao hupatikana magharibi mwa Afrika wanajulikana kwa kuheshimu miujiza.
-BBC