Raia wa Burundi Wapiga Kura Kumchagua Rais Wao

Baadhi ya raia wa Burundi wakiwa katika foleni ya kupiga kura.

Baadhi ya raia wa Burundi wakiwa katika foleni ya kupiga kura.


UCHAGUZI wa Rais umeanza Burundi baada ya kumalizika kwa ghasia na maandamano ya miezi kadhaa iliyopita, hatimaye raia wa Burundi wamepiga kura ili kumchagua rais wao. Hata hivyo watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika Mji Mkuu wa Bujumbura.

Vyombo vya habari vya kimataifa vinasema kuwa, milio ya risasi na gruneti zimesikika usiku kucha katika Mji Mkuu wa Burundi- Bujumbura. Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo aliyekuwa rais pia anawania muhula wa tatu licha ya madai ya wapinzani wake kudai anakwenda kinyume na katiba ya nchi.

Viongozi wanne wa upande wa upinzani wamesusia uchaguzi huo. Rais Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipanga foleni kabla ya kupiga kura yake katika kituo kilichokaribu na Mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura.

Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja wa Afrika katika muda wa lala salama. Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa Rais Nkurunziza.

Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Uchaguzi huu unafanyika licha ya taharuki kuhusiana na mgogoro wa kisiasa. Wagombea waliopinga uchaguzi huo ni pamoja na Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya. Jina la rais Nkurunziza na nembo ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.

Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi. Rais Nkurunziza ameonekana akipiga kura karibu na mji wa Ngozi Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo.
Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.

Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.

Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu. Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.

Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.
-BBC