Que Bac Mabingwa Mbagala Cup, Watwaa Mbuzi na Jezi

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akisalimiana na wachezaji kabla ya kipute kuanza.

Picha ya pamoja kati ya wachezaji na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John.

Mashindano ya Mbagala Cup

Mashindano ya Mbagala Cup

Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.

Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.

Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. Kushoto ni Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John.

Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia.

Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia.

mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora.

mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora.

Mchezaji bora akipokea kitita cha shilingi laki moja toka kwa mgeni rasmi Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa.

Timu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.

Timu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.

TIMU ya Vijana ya Mpira wa Miguu ya Que Bac ya Mbagala Kipati jijini Dar es Salaam jana imeibuka bingwa wa Mashindano ya Mbagala Cup baada ya kuibugiza timu ya mpira wa miguu ya Kipati magoli 2 kwa bila. Que Bac imetawazwa mabingwa na kukabidhiwa Mbuzi, seti moja ya jezi pamoja na mpira.

Que Bac ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Kipati ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji wao hatari, Yahya Tumbo (9) alikwamisha mpira katika nyavu za wapinzani baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake. Lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Que Bac walikuwa mbele kwa goli moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo wachezaji wa Kipati waliongeza mashambulizi kwa wapinzani wao kutaka kusawazisha goli lakini goli kipa wa Que Bac pamoja na walinzi wake walikuwa makini na kuondoa hatari zote mara kadhaa langoni mwao.

Jahazi la Kipati lilizamishwa zaidi na mshambuliaji wa Que Bac, Shine Duu jezi namba 17 ambaye alifanikiwa kuifungia timu yake goli la pili na kuongeza matumaini ya kutangazwa Mabingwa wa Mashindano hayo (Mbagala Cup). Hadi kipenga cha mwisho Que Bac 2 na Kipati 0.

Akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali, Mratibu wa Mashindano hayo, Musa Hemed (Kibwetele) alisema mashindano hayo yalianza rasmi Aprili 5, 2014 ambapo timu 16 zilishiriki katika mashindano huku zikiwa katika makundi mawili, yaani A na B na kila kundi lilikuwa na timu nane. Alisema mshindi wa pili katika mashindano hayo amefanikiwa kupata seti moja ya jezi pamoja na mpira, huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji na timu yenye nidhamu.

Alisema lengo la mashindano hayo ilikuwa kuwakuza vijana katika vipaji vyao kwenye fani ya mpira wa miguu pamoja na kuwaunganisha vijana kushiriki katika michezo kwa pamoja. “…Sisi eneo letu tumezoea kuona mashindano ambayo yanaanzishwa labda na diwani lakini tena mara moja kwa muda mrefu. Sasa mimi nikakaa na kufikiria nasie vijana tunaweza kujipanga na kuanzisha mashindano kama hayo,…nikazialika timu tukachangishana ada kidogo na hatimaye tukapata mlezi wa mashindano na yamefanyika,” alisema Kibwetele.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa ameahidi kuyafadhili mashindano hayo kuanzia sasa na atakuwa akiwezesha kufanyika kwake.
Mbali na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo.

Naye Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John alisema lengo la mashindano hayo ni kutaka kuwaleta vijana karibu, kuleta upendo dhidi yao na kudumisha umoja na amani kwa vijana wote. Alisema mashindano kama hayo yanawatoa vijana kutoka katika mtizamo ya wao kukaa vijiweni na kujishughulisha na michezo zaidi ambayo inamanufaa kwao kuliko kushinda wakipiga soga kwenye makundi vijiweni. Zimeshiriki Kata tano za Kata ya Mbagala, Kata ya Kiburugwa, Kata ya Kijichi, Mbagala Kuu

“Unajua vijana wengi mitaa yetu wanakaa vijiweni si kwamba wanapenda kufanya hivi, wanafanya tu kwasababu wanakosa cha kufanya…sasa kuna kila sababu watu wenye nafasi kujitokea na kuwawezesha ili kuwatoa walipo, nimetokea mimi nimedhamini mashindano yamefanyika, wameshindana na vijana wamepata burudani, upendo na amani pia mshindi kapatikana,” alisema.

Aidha alisema wapo vijana wengi wenye vipaji ambao wanaitaji kupewa nafasi za kushiriki katika mashindano kama hayo na hatimaye vipaji vyao kuonekana na kuendelezwa katika mashindano ya juu. “…Tumeona leo hapa vijana wameondoka na zawadi mbalimbali wachezaji bora wamezawadiwa, timu bora, golikipa bora kapatikana, timu zimejishindia jezi na mipira vyote vyao…timu hizi awali zilikuwa zikicheza na jezi za kukodisha lakini leo wamepata za kwao baada ya kushinda,” alisema.

Kijana huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya kupunguza maovu kwa vijana kwani katika kipindi chote cha mashindano hayo vijana walielekeza nguvu zao nyingi kwenye michezo kimashindano jambo ambalo anaamini limepunguza baadhi wenye nia ovu kubadili mienendo yao kutokana na mashindano hayo. Pamoja na hayo aliishauri Serikali na vyama vya soka kushuka ngazi ya chini mitaani kusaka vipaji vya michezo anuai kwani zipo vingi lakini vinakosa fursa ya kuonekana.