Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi Tanzania leo jijini Dar es Salaam limepokea msaada wa kamera 20 na vitabu 100 vyenye thamani ya sh. milioni 30, ilivyopewa na kampuni ya Puma wasambazaji wa mafuta nchini.
Akipokea vifaa hivyo leo, Kamishna wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, ASP-Paul Chagonja amesema vifaa hivyo vitalisaidia jeshi hilo kukabiliana na vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kupambana na wanaovunja sheria za usalama barabarani.
Aidha amezitaka kampuni nyingine na jamii kuiga mfano wa watu kama hao ambao wanajitokeza kulisaidia jeshi la polisi ili kuweza kutimiza wajibu wake ipasavyo.
Ameongeza kuwa mtazamo wa kampuni hiyo unakwenda sambamba na suala zima la kulinda raia na mali zake hivyo kubainisha vifaa hivyo pia vitatumika kufanya uchunguzi ajali zinapotokea.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Puma, Maregesi Manyama amesema kampuni yake imeamua kutoa msaada huo kwa Jeshi la Polisi ili visaidie kudhibiti ajali ambazo zinaweza kuzuilika.