PSPF Zanzibar Wasaidia Waliopatwa na Maafa

Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.

Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo
la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya
mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja
vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.

PSPF Zanzibar Wasaidia Waliopatwa na Maafa

 OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya
Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za
masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa
uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa
makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe
chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake
kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali
wananchi wakati wa maafa
  na kutowa
shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika
katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.

WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.

Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.