PSPF Yawakutanisha Wadau kwa Chakula cha Usiku

Mkurugenzi  wa Mipango na Uwekezaji PSPF, Gabriel Silayo akieleza namna mfuko unavyowekeza ili kulinda thamani ya michango ya wanachama dhidi ya mfumuko wa bei na changamoto nyingine za kiuchumi.

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji PSPF, Gabriel Silayo akieleza namna mfuko unavyowekeza ili kulinda thamani ya michango ya wanachama dhidi ya mfumuko wa bei na changamoto nyingine za kiuchumi.

Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PSPF, Adam Mayingu akitoa taarifa za
majukumu, mafanikio, changamoto na mipango ya mfuko kwa wadau wa mfuko
huo waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na
PSPF.
Wakurugenzi  wa idara tano za PSPF katika picha ya pamoja wakati wa utambulisho kwa wadau wa mfuko huo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Gabriel Silayo, Kaimu Mkurugenzi wa Technohama, Andrew Mkangaa, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Francis Mselemu na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Masha Mshomba.  
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF, Francis Mselemu akifafanua jambo kwa wadau wa mfuko huo.
Ofisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke na Mshereheshaji wa hafla hiyo Ephraim Kibonde.
Mkurugenzi  wa Fedha na Utawala PSPF, Masha Mshomba akifafanua jambo kwa wadau wa mfuko huo waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni.

Ofisa  Mahusiano wa PSPF, Fatma Elhagy akifafanua jambo kwa mdau wa mfuko huo wakati wa halfa ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu  Mkurugenzi wa Technohama PSPF, Andrew Mkangaa akieleza namna mfumo wa habari na mawasiliano unavyotumika katika kuboresha huduma za mfuko katika utunzaji wa kumbukumbu, ukokotoaji wa mafao, kuandaa malipo ya mafao na mawasiliano ya ndani na nje.
Mkurugenzi  wa Ukaguzi wa Ndani PSPF, Godfrey Ngonyani akieleza shughuli za ukaguzi  wa ndani zinavyofanyika kwa uangalifu ili kuongeza ufanisi na utendaji wa mfuko.
Wadau wa mfuko wa PSPF.
Meneja  wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin akitoa maelezo juu ya mpango wa uchangiaji wa hiari na namna wadau na jamii kwa  ujumla inavyoweza kunufaika na mafao yanayopatikana katika mpango huo.
 Wadau wa mfuko wa PSPF.
 Baadhi ya watumishi wa PSPF.
  Wadau wa PSPF.